1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali bado tete nchini Syria

7 Julai 2011

Waandamanaji nchini Syria wameingia tena katika miji kadhaa ya jiji la Hama nchini Syria ambao umekuwa ukilengwa na vikosi vya usalama nchini humo baada ya tukio lililosababisha kiasi cha watu 20 kuuwawa hapo awali.

https://p.dw.com/p/11qmT
Waandamanaji nchini SyriaPicha: picture-alliance/dpa

Jana usiku waandamanaji walionekana katika al-Aswad na al-Hajar karibu na mji mkuu wa Damascus pamoja na upande wa magharibi wa jimbo la Homs. Wote kwa namna tofauti walikuwa wakishiishinikiza serikali ya nchi hiyo kusimamisha ukandamizaji wa vikosi vya usalama na jeshi la nchi hiyo kulizingira jiji la Hama.

Kwa mujibu wa wanaharakati wa haki za binadamu kiasi cha watu 23 waliuwawa katika machafuko yaliyoteka Hama, mji huo ndiyo kiiini cha maandamano makubwa dhidi ya utawala wa rais Bashar al-Assad.

Hata hivyo Shirika la Habari la hapa Ujerumani DPA linasema imekuwa vigumu kuhakiki ripoti hiyo ya vifo kwa kuwa serikali ya Syria imepiga marufuku vyombo vya habari vya kigeni kuingia nchini humo.

Serikali ya Syria imevishutumu vile ambavyo imeviita" vikundi vya wachochezi" kwa kuzuia barabara na kuchoma moto matairi.

Syrien Demonstration Facebook
Vikosi vya usalama SyriaPicha: picture-alliance/dpa

Televisheni ya serikali imemnukuu afisa mmoja wa serikali wa nchi hiyo akisema majeshi ya serikali yameingia katika miji ya jiji hilo kurejesha hali ya utulivu na usalama baada ya vitendo vya kuzuia barabara na hujuma nyingine zilizokuwa zikifanywa na waandamanaji hao.

Nayo televisheni ya Al Arabiya imemuonesha mkazi mmoja amabea hakuweza kutambulika kwa mara moja akisema vikosi vya uslama vimeongeza nguvu zake katika maeneo ya Hama.

Bwana huyo amesema ulinzi zaidi umehimarishwa katika makao makuu ya chama tawala cha nchi hiyo, (Baath Party) pamoja na makao makuu ya polisi.

Baadhi ya wanaharakati wametoa mitazamo yao kuhusu juu ya hali ya mambo inavyoendelea nchini Syria.

Akitolea mfano wa maandamano ya ijumaa iliyopita, Rami Abel Rahman kiongozi wa waangalizi wa Kisirya waliopo nchini Uingereza amesema amesema vikosi vya usalama na vikundi vinavyopinga serikali, katika Homes vilishambuliana kwa risasi.

Amesema watu hao wamesema wapo tayari hata kupoteza maisha katika kuulinda mji wao.

Mwanaharakati mwingine anasema maandamano hayo yaliyofanywa na kiasi cha watu laki tano, yalikuwa ya amani kwa asilimia 100. Hata hivyo kiasi ya wana usalama 80 walijeruhiwa na vikundi vya raia wenye silaha.

Marekani ilisema hakuna ushahidi wa kutosha kwamba baadhi ya waandamanaji hawana silaha lakini imetoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuondoa vikosi vyake katika mji wa Hama.

Hama ni kitovu cha vuguvugu la mageuzi nchini Syria ambapo mwaka 1982 kulitokea na tukio la umwagikaji damu liliacha kiasi ya watu 20,000 kupoteza maisha wakati wa zama za baba wa rais Bashar, marehem Hafez al-Assad.

Mwandishi: Sudi Mnette/AFP

Mhariri:Yusuf Saumu