1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali inasikitisha baada ya zilzala nchini Peru

18 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBY6

Lima:

Baada ya zilzala iliyopiga nchini Peru,rais wa nchi hiyo Alan Garcia ameamuru wanajeshi wapige doria katika maeneo ya maafa ili kuepusha visa vya wizi na kupora mali.Rais Garcia anazingatia pia uwezekano wa kutangaza marufuku kwa watu kutoka saa za usiku.Picha zilizonaswa na televisheni kutoka maeneo yaliyoathirika kwa tetemeko la ardhi katika mwambao wa kusini wa bahari ya Pcific zinaonyesha watu waliokata tamaa wasiojua la kufanya,wakivamia maduka na kuzuwia malori ili kujipatia chakula.Wahka umezidi kufuatia zilzala zaidi katika eneo hilo.Duru za maafisa wa serikali zinasema maiti 500 zimefukuliwa baada ya zilzala iliyopiga jumatano iliyopita.Maelfu wengine wamevunjikiwa na nyumba zao.