1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali katika Gaza

Oumilkher Hamidou24 Januari 2009

Umoja wa Ulaya wapanga kuanza haraka kuijenga upya Gaza

https://p.dw.com/p/GfLL

Cologne/Brussels:


Umoja wa Ulaya umeitaka Israel ifungue mipaka yote ya kuingia Gaza."La muhimu zaidi kwa sasa ni kuhakikisha wakaazi milioni moja na nusu wa eneo hilo wanapatiwa mahitaji muhimu",amesema hayo muakilishi mkuu wa siasa ya nje wa Umoja wa Ulaya,Javier Solana kupitia kituo cha matangazo cha Deutschlandfunk mjini Cologne.Kwa mujibu wa mwanadiplomasia huyo ,Umoja wa Ulaya unataka kuanza haraka kusaidia kujenga upya maeneo ya wapalastina-unapinga lakini ushirikiano wa moja kwa moja pamoja na Hamas wanaolitawala eneo hilo.Javier Solana anapigania uchunguzi wa kimataifa ufanywe baada ya wiki tatu za hujuma za Israel huko Gaza,ili kufichua kama uhalifu wa vita umefanyika.Kwa upande wake Ufaransa imetuma manuari katika fukwe za Gaza -ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuunga mkono mpango wa kuweka chini silaha.Manuari hiyo inayobeba helikopta itakua ikipiga doria kuzuwia silaha zisiziingizwe kichini chini huko Gaza.