1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali mjini Mombasa ni shwari baada ya ghasia za siku tatu

30 Agosti 2012

Hali Mjini Mombasa nchini Kenya inasemekana kuwa shwari kufuatia ghasia zilizoanza siku ya jumatatu baada ya kuuwawa kwa kiongozi wa kidini anayehusishwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab sheikh Aboud Rogo Mohammed.

https://p.dw.com/p/1605Y
Mji wa Mombasa ulikuwa na vurugu baada ya kifo cha Sheik Aboud Rogo
Mji wa Mombasa ulikuwa na vurugu baada ya kifo cha Sheik Aboud RogoPicha: Getty Images

Tangu kuuwawa kwa kiongozi huyo kumekuwa na ghasia za hapa na pale mjini Mombasa, Tayari watu 24 wamefikishwa mahakamani kufuatia ghasia hizo. Kwa sasa serikali imeunda jopo la watu 11 kuchunguza mauaji ya Sheikh Rogo na pia ghasia zilizosababisha mauaji ya watu wanne wakiwemo maafisa watatu wa polisi.

Amina Abubakar amezungumza na mwandishi wetu wa Mombasa Eric Ponda juu ya hali halisi ya mambo kwa sasa

(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi Amina Abubakar

Mhariri Mohammed Abdul-Rahman