1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ni shuwari mkatika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo

28 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyT

Kampeni ya uchaguzi wa rais katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo imemalizika jana katika hali ya hofu na wasi wasi baada ya machafuko ya siku moja kabla kati ya wafuasi wa rais anaemaliza wadhifa wake Joseph Kabila na mpinzani wake,makamo wa rais Jean-Pierre Bemba.Mikutano ya hadhara iliyokua iitishwe imefutwa kutokana na sababu za usalama.Hali jumla inasemekana kua shuwari nchini humo .Watu wasiopungua watano wameuwawa alkhamisi iliyopita katika maeneo ya mikoani ambako takriban kila siku machafuko yamekua yaakiripootiwa tangu kampeni za duru ya pili ya uchaguzi zilipoanza kati kati ya mwezi huu.Naibu msemaji wa tume ya Umoja wa mataifa katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo-MONUC,Jean-Tobie Okala amewatolea mwito wakongomani wasikubali kushawishiwa.”Bwana Jean-Tobie Okala amewataka watetezi wote wawili,watoe mwito kama huo kwa wafuasi wao.