1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ni tete Burundi huku uchaguzi wa rais ukikaribia

Josephat Nyiro Charo16 Juni 2010

Tangu jana saa 12 jioni wafuasi wa chama FNL wamekusanyika nje ya nyumba ya Agathon Rwasa kuwazuia askari polisi wa serikali wasimkamate kiongozi huyo

https://p.dw.com/p/NsBR
Warundi wakipiga kura wakati wa uchaguzi wa mitaaPicha: DW

Huko nchini Burundi, kuna taarifa kuwa wafuasi wa chama kikuu cha upinzani cha FNL, wameizingira nyumba ya kiongozi wao Agathon Rwasa kwa nia ya kuzuia jaribio linalosemekena ni la serikali kutaka kumkamata kiongozi huyo. Bwana Rwasa ni miongoni mwa viongozi wa upinzani waliotangaza kuususia uchaguzi mkuu ujayo wa urais nchini Burundi.

Polisi ilifiatuwa hata risasi kuwatawanya raia hao na kumuokoa mmoja wao aliyekuwa kavamiwa na umati wa watu wafuasi wa chama cha FNL. Agathon Rwasa amesema haelewi sababu za kutaka akamatwe. Mwanasheria mkuu amesema hakuna waranti waliosaini wa kutaka akamatwe.

Kutoka Bujumbura mwandishi wetu Hamida Issa ametutumia taarifa ifuatayo.

Mwandishi:Hamida Issa

Mhariri: Josephat Charo