1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali Visiwani Komoro

26 Machi 2008

Uvamizi uliofanywa na majeshi ya Komoro na yale ya Umoja wa Afrika,AU, katika Kisiwa cha Anjouan, kumuondosha madarakani mtawala mweusi wa kisiwa hicho, Kanali Mohamed Bakari, umefanikiwa.

https://p.dw.com/p/DUlc
Wanajeshi wa Tanzania kisiwani AnjouanPicha: AP

Majeshi hayo ya Komoro na pia yakiwemo kutoka Tanzania na Sudan, yameidhibiti hali ya mambo katika Anjouan, hivyo kutimiza ile ahadi alioitoa Rais Abdullah Sambi wa Komoro kwamba uasi uliofanywa huko Anjouan utamalizika karibuni.

Othman Miraji, alizungumza kwa simu na Salim Himid, waziri wa zamani wa mambo ya kigeni wa Visiwa vya Komoro, na kumuuliza sasa Visiwa vya Komoro vinaelekea wapi?