1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya Kisiasa Zanzibar

20 Mei 2008

Nchini Tanzania chama tawala CCM na kile cha upinzani CUF, bado vimo katika mvutano kuhusu njia za kuondoa mpasuko wa kisiasa kisiwani Zanzibar.

https://p.dw.com/p/E36p
Rais Aman Abeid Karume wa ZanzibarPicha: AP Photo

Jana katika mkutano na waandishi habari Rais Amani Karume alisema atakuwa tayari kukutana na Katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif hamadi pindi tu CUF Itamtambua kuwa ndiye rais wa visiwa hivyo. Pamoja na hayo akatetea uteuzi wake wa Waziri mmoja tu kutoka Pemba akisema huko alikochaguliwa na idadi ndogo sio sawa na katika kisiwa cha Unguja.

Nimezungumza kwa njia ya simu na mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mhadhiri katika chuo kikuu cha Dar es salaam Profesa Mwesiga Baregu na nilimuuliza kwanza maoni yake juu ya matamshi hayo ya Rais Karume.