1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya Mjerumani mtekwa nyara nchini Afghanistan inazidi kuwa mbaya

Maja Dreyer24 Julai 2007

Wanamgambo kumi wa Taliban waachiliwe huru na wanajeshi wa nje watoke Afghanistan– hilo ndilo dai la kundi la wateka nyara lilomteka Mjerumani mmoja, Waafghanistan wanne na watu 23 raia wa Korea Kusini nchini Afghanistan. Wakati huo huo, hali ya Mjerumani mwingine inazidi kuwa mbaya, baada ya maiti ya Mjerumani aliyekufa kifungoni kurejeshwa Ujerumani.

https://p.dw.com/p/CHAe
Picha: AP

Ni siku saba tangu Wajerumani wawili pamoja na wenzao wa Kiafghanistan walipotekwa nyara. Juzi maiti ya Mjerumani mmoja imepatikana na kurejeshwa Ujerumani. Wizara ya nje ya Ujerumani imethibitisha kuwa maiti ina majeruhi kadhaa ya kupigwa risasi, lakini kulingana na serikali za Berlin na Kabul zimesema amekufa kutokana na hali ngumu ya kifungo. Mjerumani mwingine mhandisi na wenzake wanne wa Afghanistan bado wako hai, lakini Mjerumani anaugua. Haya ni kulingana na msemaji wa kundi la Taliban, Yussif Ahmadi, aliyasema pia mhandisi huyu ana ugonjwa wa sukani lakini kundi la waasi halina dawa.

Mahala walioko watekaji na waliotekwa nyara panajulikana. Kama Wakorea 23 wa kundi la Wakristo wa kuleta msaada wote wametekwa nyara Kusini mwa Afghanistan. Sababu ya matukio haya lakini ni tofauti. Kundi la Taliban limearifu kuwa muda wa mwisho uliotolewa kuwaua Wakorea umerefushwa hadi leo saa nane na nusu saa za UTC.

Idara za serikali husika zinafanya bidii kubwa mazungumzo na watekaji nyara yaendelee, kama anavyoeleza naibu waziri wa ndani wa Afghanistan, Abdul Hadi Khalid: “Tumeunda tume maalum ya serikali. Tume hiyo ina wajibu wa kiserikali na imepewa mamlaka ya kuzungumza na watekaji nyara.”

Pamoja na tume hiyo, wazee na wasomi wa Afghanistan walihusishwa katika juhudi za kuwaokoa Wakorea hao 23.

Msemaji wa Taliban Ahmadi alisema baada ya Ujerumani kukataa kuondosha jeshi lake, waasi sasa wanataka wanamgambo kumi wa Taliban waachiliwe huru. Hata hivyo lakini, kuna mashaka juu ya jukumu la Taliban katika utekaji nyara huo. Msemaji huyu huyu, kwa muda wa siku mbili alisisitiza Wataliban waliwaua wafungwa wao wote. Jana lakini amebadilisha hadithi yake kuwa sawa na taarifa za serikali ya Afghanistan, yaani kwamba Mjerumani mmoja na Waafghanistan wanne bado wako hai.

Kuna habari nyingine zinazosema kuwa kundi la wanamgambo wa Pashtu wanahusika ambao wana malengo ya kihalifu na si ya kisiasa.

Kamanda wa jeshi la ISAF nchini Afghanistan, Dan McNeill, anaamini Wataliban wana mbinu fulani wakitumia kesi hizo za utekaji nyara: “Nadhani ni jambo la kuvutia kweli: bunge la Ujerumani Bundestag linatarajiwa kupiga kura baadaye mwaka huu juu ya hatua ya kijeshi nchini Afghanistan. Tunakumbuka utekaji nyara wa waandishi wa habari kutoka Italy siku chache tu kabla ya uchaguzi nchini humo. Na wa Wafaransa kabla ya uchaguzi nchini mwao. Huenda ni mkakati fulani ya waasi.”

Wakati mazungumzo yanaendelea, serikali ya Afghanistan imearifu kuwa wanamgambo 75 wanaoaminika kuwa Wataliban waliuawa katika mapigano katika maeneo mbalimbali Kusini mwa nchi hiyo.