1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya mpakani baina ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Uganda

16 Agosti 2007

Iliripotiwa karibuni kuweko hali isiokuwa tulivu katika mpaka baina ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, na baada ya kufanya mazungumzo punde hivi huko Kinshasa, waziri wa mambo ya kigeni wa Uganda, Sam Kutesa, alisema nchi mbili hizo zitafanya mkutano katika mji wa mpakani mwishoni mwa mwezi huu kuendeleza mdahalo. Alisema njia za mawasiliano zimefunguliwa kutanzua visa vyovyote vya baadaye.

https://p.dw.com/p/CH9V

Alisema jeshi la nchi yake litaitetea ardhi ya Uganda dhidi ya mtu yeyote atakayeingia nchini humo kwa nguvu. Ilitajwa hapo awali kwamba raia watatu wa Uganda na mfanyakazi wa kampuni ya Kiingereza inayochimbua mafuta katika eneo la Ziwa Albert waliuliwa na wanamgambo waliovuka mpaka kutokea Kongo.

Othman Miraji alizungumza na waziri wa habari wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Toussent Chirombo, kutaka kujua hali ilivyo baina ya nchi hizo mbili.