1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya mtafaruku yatanda Kenya

29 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/Chsx

NAIROBI

Chama cha Upinzani nchini Kenya kinachoongozwa na Raila Odinga ODM kimedai ushindi katika uchaguzi mkuu.

Akidai ushindi wa chama hicho Mgombea mwenza wa raila Odinga bwana Musalia Mudavadi amesema kutokana na tume kuchelewesha matokeo ya urais ni wazi kwamba raila Odinga ndie rais mpya wa Kenya na hivyo bwana Mwai Kibaki inambidi akubali Kushindwa.Hata hivyo mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi bwana Samuel Kivuitu akizungumzia kuhusu kucheleweshwa kwa matokeo hayo amesema hajafahamu ni kwanini baadhi ya vituo havijatoa matokeo na wanapojaribu kupiga simu kuuliza simu hizo zimefungwa.

Hali hiyo imetajwa kuwaghadhabisha wakenya na kuzusha ghasia katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo ambapo watu wawili wameuwawa kwa kupigwa risasi na Polisi mjini Nairobi.Mapema leo hii wafuasi bwana Raila Odinga waliwasha moto na kuandamana katika maeneo kadhaa kupinga hatua ya tume ya uchaguzi.

Matokeo ya mwanzo yanampa ushindi wa wazi bwana Raila Odinga akiwa na asilimia 49 ya kura zilizohesabia dhidi ya rais Mwai Kibaki aliyepata asilimia 45. Upinzani lakini unadai kwamba kuna hila kutoka upande wa serikali za kuiba kura na kumpa ushindi rais Mwai Kibaki anayewania muhula wa pili madarakani.Ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi huo kutoka Umoja wa Ulaya imetoa mwito kwa wakenya kuacha vurugu na kusubiri matokea kamili yatakayotangazwa na Tume ya Uchaguzi.