1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya Syria bado sio Shwari

27 Februari 2012

Watu watatu wameuwawa katika mashambulio ya mizinga ya majeshi ya serikali huko Syria katika mji wa Homs huku matokeo ya kura ya maoni ya tarehe 26 Februari juu ya katiba mpya yakitarajiwa kutangazwa.

https://p.dw.com/p/14Ab8
Moto bado unawaka Syria
Moto bado unawaka SyriaPicha: AP

Hali ya mambo bado inaonekana kuwa mbaya nchini humo wakati ambapo pamoja na jitihada nyingine Shirika la Msalaba Mwekundu limesema litajaribu kuingia katika mji wa Baba Amr kuwaokoa waandishi habari wawili waliojeruhiwa katika mashambulio ya makombora pamoja na watu wengine wanaohitaji msaada katika eneo hilo.Shirika hilo limekuwa katika majadiliano ya kujaribu kupata idhini ya serikali ya kuingia katika eneo hilo kuwaokoa waandishi habari hao raia wa Uingereza Paul Conroy na raia wa Ufaransa Edith Bouvier.

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amesema jitihada za kuwakomboa wanadishi habari hao wawili zinaelekea kufanikiwa.Wanaharakati wanasema idadi ya waliouwawa imefikia watu 60 huku wengi wakiuwawa katika mji wa Homs.Kauli nyingine juu ya hali ya mambo nchini Syria imetolewa huko Moscow na waziri mkuu wa Urusi Vladmir Putin akiizikosoa nchi za Magharibi kwa msimamo kuikandamiza serikali ya Syria.

Urusi na China dhidi ya Wamagharibi

Aidha waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov pia amezilimbikizia lawama nchi za magharibi kwa kufanya mkutano wa Tunis nchini Tunisia ulioegemea upande mmoja wa mzozo wa Syria.Nchi za Kiarabu zilitoa kilio cha kutaka nchi za magharibi ziingilie kati mzozo wa Syria lakini kuhusu kuwapa silaha wapinzani wa Assad Marekani imeonekana kulipinga wazo hilo.Kama ilivyojitokeza kwenye kauli ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton aliyesema.

Waziri mkuu wa Urusi Vladmir Putin
Waziri mkuu wa Urusi Vladmir PutinPicha: Reuters

''Kwanza kabisa hatujui nani wakupewa silaha nchini Syria,Tunafahamu kwamba kiongozi wa Al Qaeda Zawahiri anawaunga mkono wapinzani nchini Syria,je tunaunga mkono Alqaeda nchini Syria?Hamas sasa linaunga mkono upinzani,Je sisi tunaliunga mkono kundi la Hamas nchini Syria?''

China imemkosa waziri huyo mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton kwa kauli yake ya kuzikosoa China na Urussi kwa msimamo wao juu ya Syria ikisema haikubaliki.Clinton amezikasirisha Urusi na China baada ya kuzishutumu nchi hizo kwamba zinahujumu matakwa sio tu ya Wasyria bali hata harakati za za kudai demokrasia katika nchi za Kiarabu.

Wapinzani Syria walalamikia katiba mpya
Wapinzani Syria walalamikia katiba mpyaPicha: AP

Katiba mpya ya Syria

Juu ya hayo matokeo ya kura ya maoni juu ya katiba mpya pia yanasubiriwa hii leo ambapo ikiwa ni hatua itakayofungua njia kwa vyama vingine vya kisiasa nchini humo mbali na chama cha Baath cha rais Bashar al Al Assad kilichoko madarakani tangu mwaka 1963.Lakini wapinzani wana atiati juu ya katiba mpya Wakidai,

''Tatizo ni kwamba wahusika hawaheshimu sheria,kwahivyo haijalishi katiba mpya itakuwa vipi,mradi wapo madarakani mageuzi haya hayatokuwa na maana yoyote''

Kumeshajitokeza mgawanyiko ndani ya baraza la kitaifa la Syria ambalo ni upinzani,baada ya wanachama wake 20 kuunda kundi jingine lililojitenga.

Mwandishi: Saumu Yusuf

Mhariri: Mohammed AbdulRahman