1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya watoto nchini Lebanon

Abdulrahman, Mohamed4 Machi 2008

Kwa miaka mingi watoto nchini Lebanon wamekabiliwa na vita na mabomu kiasi ya kwamba machafuko na matumizi ya nguvu yamegeuka kuwa sehemu ya maisha yao.

https://p.dw.com/p/DHv9
Abdul-Kadir Abdullah mwenye umri wa miaka 4, akiwa na dada yake Lilaf, miaka 8 mjini Beirut.Picha: AP

Hali inazidi kuwa ya hatari kutokana na uhasama baina ya makundi yanayopi´ngana nchini Lebanon na maisha ya watoto nchini humo kuzidi kukabiliwa na kitisho.

Vita vya 2006 vilisababisha zaidi ya watu 1,200 kuuawa, robo moja ya wakaazi kutawanyika na hasara ya mabilioni ya dola kwa taifa hilo lenye mzigo mkubwa wa madeni. Kitisho kimoja cha ugaidi baada ya kingine na hali hiyo imeshindwa kuleta utulivu na hivyo watoto ambao ni theluthi moja ya idadi ya wakaazi wapaatao milioni 4 wanaayashuhudia maisha yao yakififia taratibu.

Afisa mawasiliano wa Shirika la kuwahudumia watoto la umoja wa mataifa-UNICEF- Soha Basat, anasema kiasi ya theluthi moja ya umma wa Lebanon ni watu waliotawanyika kutokana na mgogoro na vita kati ya Israel na wapiganaji wa Hezbollah.

Wengi wao ni watoto. Karibu miaka miwili baada ya vita,familia nyingi zinashindwa kurudi katika makaazi yao.

Mbali na ukosefu wa matumaini ulio wazi kwa watoto, lakini pia wanakumbwa na matatizo ya kuweweseka usiku kutokana na waliyoyashuhudia ikiwa ni pamoja na vifo vya jamaa zao wa karibu huku wakilazimika pia kakabiliana na mazingira mapya ya maisha.

Katika kijiji cha Tayri, mtoto mmoja anasimulia jinsi alivyonusurika katika hujuma ya bomu kwenye basi moja la raia, ilioafanywa na ndege za kijeshi za Israel. Aanasema alikua akipepea shati lake jeupe kama alama ya amani, akitoa kichwa chake dirishani mwa basi hilo, wakati bomu lilipoangukia karibu na kumjeruhiwa vibaya mama yake. Kutokana na hayo , shangazi yake Ibtissam Cheito anasema wakati wowote Abbas anaposikia mlio wa ndege huwa anajificha.

Tatizo jengine mbali na vita ambalo huwakabili watoto ni ukatili wanaofanyiwa na mmoja wa wazazi na hali hiyo sana hutokana na uamsikini uliokithiri. Watoto wengi wakiume hulazimika kuacha shule ili kuzisaidia familia zao.

Utatuzi wa hali halisi ya wakati huu miongoni mwa watoto bado ni mgumu, kwa sababu ya ukosefu wa utulivu wa kisiasa. Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka minane alisikika akisema," wakati wote mama yangu anapotoka, mimi huwa na wasi wasi, kwa sababu sijui ni wakati gani atatega bomu kwenye umati wa watu." Itakuaje akidhurika ? Jee akiondoka nani ataishi na mimi.?

Kwa mtazamo wa yote hayo, watoto nchini Lebanon wanaelewa fika hatari inayowakabili kawa sababu ya ukosefu wa utulivu na usalama kwa jumla nchini mwao.