1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali yaendekelea kuwa tete nchini Yemen

2 Juni 2011

Safari za ndege zimetatizika huku ndege zikuzuiwa kutua na kuruka kutoka uwanja wa mji mkuu, Sana'a.

https://p.dw.com/p/11T9R
Moshi ukiwa umetanda katika anga ya mji wa Sana'aPicha: picture alliance/dpa

Nchini Yemen, hali inaripotiwa kuwa inatisha. Kwa sasa mapigano makali yametokea kwenye mji wa Taez na milio ya risasi inarindima kote kwenye mji mkuu wa Sana'a. Ifahamike kuwa Rais Ali Abdullah Saleh wa Yemen bado anakataa kulitia saini pendekezo la Baraza la mataifa ya Ghuba, GCC, linalompa fursa ya kujiuzulu pasina adhabu ya mahakama. Hii leo ndege zimeripotiwa kuwa zimezuiwa kutua na kuruka kutokea uwanja wa ndege wa Sana'a kwa sababu ya mapigano. Hata hivyo serikali imezikanusha taarifa hizo. Ili kuyajua yanayojiri Thelma Mwadzaya amezungumza na Sheikh Badawi mkaazi wa eneo la Hadhra-maut.

Ni Sheikh Badawi mkaazi wa eneo la Hadhra-maut.

Mwandishi:Thelma Mwadzaya

Mhariri:Josephat Charo