1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali yarejea kawaida Thailand

Thelma Mwadzaya3 Desemba 2008

Waandamanaji wanaopinga serikali nchini Thailand wameondoka kwenye viwanja viwili vikuu vya ndege mjini Bangkok baada ya kuvizingira tangu wiki iliyopita

https://p.dw.com/p/G86T
Waandamanaji wa chama cha People's Alliance for Democracy,PAD wakisherehekea ushindi waoPicha: AP


Ushindi wao huo umefanikishwa na uamuzi wa mahakama ya katiba uliomlazimisha Waziri mkuu Somchai Wongsawat kujizulu.Kwa sasa viongozi waliongolewa madarakani wanakutana kujadili hatua ya kumteua kiongozi wa muda nchini humo.


Kiongozi wa upinzani wa chama cha Democratik nchini humo Appisyed Vechasiwat anasisitiza kuwa nchi hiyo inahitaji uongozi bora


Suala tete linalosubiri ufumbuzi ni atakayekuwa madarakani nchini Thailand kwa sasa baada ya Waziri Mkuu kujiuzulu jambo ambalo huenda likazua ghasia zilizo na misingi ya kisiasa.


Hata hivyo chama cha Peoples Alliance for Democracy PAD kimetisha kusababisha vurugu endapo madai yao hayatotimizwa.


Kwa upande mwingine msemaji wa Shirika la Ndege la kitaifa la Thai Airways Ajcharnaporn na Songhkla amesema kuwa ndege ya kwanza ya abiria itaondoka saa nane mchana za Thailand ikitokea kisiwani Phuket.Ndege hiyo itatua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Suvarnabhumi