1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas lapendekeza kipindi cha kutoshambuliana na Israel

Kalyango Siraj25 Aprili 2008

Israel yasema hiyo ni 'danganya toto'

https://p.dw.com/p/DoUt
Kiongozi wa Hamas , Khaled Mashaal,akizungumza na waandishi habari mjini Damascus, Syria, Jumatatu ya April 21, 2008. Ingawa Mashaal alikariri msimamo wa Hamas wa kutoitambua Israel hata hivyo kundi hilo limependekeza kipindi cha miezi sita ya usitishwaji hujuma na Israel. Israel imelipinga wazo hilo,ikisema kuwa Hamas inataka kutumia mda huo ili kujihami zaidiPicha: AP

Kundi la Hamas linaloongoza eneo la Gaza limesema liko tayari kuheshimu kipindi cha miezi sita ya usitishwaji mashambulizi na Israel ikiwa nayo itaondoa vizuizi ilivyoiwekea eneo hillo.Lakini Isreal imepinga wazo hilo ikisema mda huo utalifanya kundi hilo kuweza kujihami zaidi.

Kundi la kipalestina la Hamas limetoa pendekezo hilo la mda wa miezi sita ambao ni tulivu katika eneo la Gaza na baadae linaweza kulihusu eneo la Ukanda wa Magharibi wa mto Jordan.

Waziri wa zamani wa mashauri ya kigeni wa Palestina Mahmoud Zahhar,amesema kuwa pendekezo la kutoshambuliana litahusu pia kuondoa mzingiro wa Israel dhidi ya Gaza.

Lakini pendekezo hilo limekataliwa na Israel.Msemaji wa serikali ya Isreal amesema kuwa pendekezo la Hamas ni ujanja tu wa kutaka kulipa kundi hilo nafasi ya kujuhami zaidi.

Kundi hilo limesema katika kipindi hicho litasitisha uvurumishwaji wa maroketi kwa makazi ya Israel nayo kwa upande wake itoe mzingiro dhidi ya ukanda wa Gaza.Afisa mmoja wa kundi la Hamas ,Ismail Radwan,ameliambia shirika la habari la AFP akiwa mjini Cairo nchini Misri kuwa pendekezo lenyewe linaweza kuitwa la nipe ni kupe.

Miongoni mwa mengine pendekezo la hamas linasema kuwa wakati Israel italipinga hilo,Misri ingefungua mpaka wake na eneo hilo hasha kituo cha kuvukia cha Rafah.Kituo hicho ndicho mlango pekee unaoelekea Gaza lakini kupitia sehemu ya Israel.Ulifungwa punde tu kundi la Hamas lilipochukua udhidibiti wa ukanda huo mwezi juni.

Kipindi kilichopita Israel imekuwa inapinga usitishwaji kwa maeneo yote ya Palestina,ikitoa hoja kuwa operesheni zake katika eneo linalokaliwa la ukanda wa magharibi ni muhimu mno katika juhudi za kuzuia mashambulizi dhidi ya taifa la kiyahudi.

Haya yote yanatokea baada ya Umoja wa Mataifa kutangaza kuwa umesimamisha shughuli zake za kuwapa msaada wa chakula wakimbizi wa kipalestina 650,000 katika Gaza kutokana na uhaba wa mafuta.

Wakati Umoja wa Mataifa ukisitisha shughuli zake na Hamas kutoa maependekezo,kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas alikuwa anakutana na rais bush wa marekani mjini Washington katika juhudi za kuleta msukumo katika mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina.Bush amesema kuwa mkakati wa utawala wake ni kupatikana kwa taifa la Palestina.

Ingawa utawala wake umebakiza miezi 10 tu katika Ikulu na pia mazungumzo yenyewe kujikokota lakini busha baado anamatumaini makubwa ya kupatikana kwa amani.

Wakati huohuo jeshi la Israel linawatafuta wanaharakati wakipalestina walioshambulia kituo cha mpaka na kuwaumiza wanajeshi wawili wa Israel alhamisi.