1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas wanasema hawataheshimu makubaliano ya kuweka chini silaha pamoja na Israel

27 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxi

TEL AVIV /GAZA:

Mashambulio ya wanaharakati wa kipalstina yamegharimu maisha ya mtu mmoja huko Sderot.Radio ya Israel imesema bwana mmoja amefariki akiwa hospitali kutokanana na majaraha.Kombora lililofyetuliwa kutoka Gaza lilipiga juu ya gari yake wakati akiwa njiani huko Sderot.Mtu mwengine alijeruhiwa.Jumla ya makombora manne yalivurumishwa dhidi ya Sderot.Wakati huo huo Hamas wanasema hawataheshimu tena makubaliano ya kuweka chini silaha yaliyofikiwa pamoja na Israel na badala yake wametoa mwito mashambulio yazidishwe.Wanaharakati hao wa itikadi kali ya dini ya kiislam wametoa mwito huo baada ya vikosi vya usalama vya Israel kuyahujumu majengo manne ya wizara ya mambo ya ndani ya Palastina yanayodhibitiwa na Hamas..Mashariki ya Jerusalem,wapalastina wawili waliokua na silaha wameuliwa baada ya kuwafyetulia risasi wanajeshi wa Israel.Na waziri wa dola wa Palastina WASFI QUBAH amekamatwa na wanajeshi wa Israel katika mji wa Jenin katika ukingo wa magharibi.