1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas wanaspinga uchaguzi wa kabla ya wakati

16 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCim

Gaza

Rais Mahmoud Abbas wa Palastina ametoa mwito wa kutishwa uchaguzi wa kabla ya wakati ili kumaliza mzozo wa kisiasa pamoja na chama tawala cha Hamas.Katika hotuba yake kwa taifa,kwa njia ya televisheni,Mahmoud Abbas amesema umma wa palastina unastahiki kuamua ili kumaliza udhia.Rais Mahmoud Abbas anapanga kuitisha uchaguzi wa bunge na ule wa rais piaWakati huo huo kiongozi huyo wa utawala wa ndani amesema kimsingi haoni shida ya kuundwa serikali ya muungano kati ya chama chake cha Fatah na Hamas.Juhudi za miezi kadhaa za kutaka kuunda serikali kama hiyo zimeshindwa hivi karibuni.Hamas wameukataa mwito wa rais Mahmoud Abbas na wameahidi kupambana na uamuzi wowote wa aina hiyo.Mshauri wa kisiasa wa waziri mkuu Ismael Haniya amesema hivi punde Hamas imewatolea mwito wafuasi wake wateremke majiani kulalamika dhidi ya mpango wa rais Mahmud Abbas wa kuitisha uchaguzi mkuu kabla ya wakati.