1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas yahitaji kuangalia mapendekezo ya Israel

Kabogo Grace Patricia24 Desemba 2009

Kundi hilo la Hamas linasubiri kupitia mapendekezo hayo katika kufikiwa makubaliano ya kuachiwa wafungwa wa Kipalestina na mwanajeshi wa Israel.

https://p.dw.com/p/LCh6
Wafuasi wa Hamas katika maadhimisho ya miaka 22 tangu kuanzishwa kundi hilo, zilizofanyika Gaza Desemba 14, 2009Picha: AP

Kiongozi wa kundi la Hamas, Mahmoud al-Sahar amesema atahitaji siku kadhaa kuangalia mwitikio wa Israel katika pendekezo lake la kubadilishana wafungwa wa Kipalestina na mwanajeshi wa Israel anayeshikiliwa na kundi hilo.

Radio ya Israel imeripoti kuwa mpatanishi wa Ujerumani amewasilisha nyaraka kwa wawakilishi wa Hamas huko Gaza, ambapo pia alifanya mazungumzo na wawakilishi hao.

Kundi la Hamas linataka kuachiwa huru kiasi Wapalestina 1,000 ili kubadilishana na mwanajeshi huyo, Gilad Shalit anayeshikiliwa na kundi hilo kwa miaka mitatu na nusu sasa.

Awali Israel ilitoa masharti kuwa zaidi ya wafungwa 100 inayowaona ni hatari sana, hawataruhusiwa kwenda katika Ukingo wa Magharibi, lakini watapelekwa tu Gaza au nje ya nchi.