1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas yakubali kusitisha mapigano, Israel yaishambulia Rafah

7 Mei 2024

Jeshi la Israel limefanya mashambulizi katika mji wa Rafah, baada ya Baraza la Vita la Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuidhinisha hatua ya kuendeleza operesheni ya kijeshi katika mji huo wa kusini mwa Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4fZrt
Wanajeshi wa Israel wakiwa kwenye mpaka wa Rafah
Askari wa Israel wamefika katika upande wa Kipalestina wa mpaka wa kivuko cha Rafah kati ya Gaza na MisriPicha: Israeli Army/AFP

Jeshi la Israel limefanya mashambulizi katika mji wa Rafah, baada ya Baraza la Vita linaloongozwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuidhinisha hatua ya kuendeleza operesheni ya kijeshi katika mji huo wa kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Marekani na Umoja wa Ulaya wameionya Israel kuhusu mashambulizi yake huko Rafah huku China ikiitaka serikali mjini Tel-Aviv kuachana kabisa na opereshi hiyo.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell, amesema licha ya hoja zinazotolewa na Israel, ni wazi kwamba mashambulizi ya Rafah yatasababisha vifo zaidi vya raia. Jeshi la Israel limechukua pia udhibiti wa kivuko cha Rafah, ambacho kimekuwa kikitumiwa kuingiza misaada Gaza.

Soma pia: Biden amuonya Netanyahu operesheni ya ardhini mji wa Rafah

Hayo yanajiri saa chache baada ya Kundi la Hamas kukubali pendekezo la wapatanishi kuhusu kusitishwa mapigano.