1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas yamteka nyara msaidizi mkuu wa serikali

15 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cbxo

GAZA CITY

Wanamgambo wa kundi la Hamas wamemteka nyara msaidizi mwandamizi wa serikali ya Rais Mahamoud Abbas wa Wapalestina.

Hamas imesema vikosi vyake vimemchukuwa Omar al- Ghoul kutoka nyumbani kwake kwa kile kinachoonekana kuwa kutekwa nyara kwa afisa mwandamizi kabisa tokea Hamas kundi la itikali kali za Kiislam kuutwaa Ukanda wa Gaza hapo mwezi wa Juni baada ya kuvishinda vikosi vya mahasimu wao wa kundi la Fatah la Rais Abbas.

Hatua hiyo imekuja katika siku hiyo hiyo ambapo waombolezaji watatu wa Fatah kuuwawa katika mripuko wa bomu kwenye maandamano ya mazishi na kuchochea mvutano kati ya makundi hayo mawili katika Ukanda wa Gaza.

Hamas leo inajiandaa kuadhimisha miaka 20 ya kuasisiwa kwa kundi hilo kwa maandamano makubwa katika Ukanda wa Gaza.

Wakati huo huo Marekani inatazamiwa kuupatia uongozi wa msimamo wa wastani wa Wapalestina chini ya Rais Abbas zaidi ya dola milioni 500 katika mkutano wa kimataifa wa wafadhili unaofanyika mjini Paris Ufaransa mwishoni mwa juma.