1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAMBURG: Iran isizidishe mvutano kuhusu wanamaji

31 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCDj

Waziri wa masuala ya nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier ameionya serikali ya Iran kutozidisha mvutano kuhusika na mgogoro wa wanamaji wa Kingereza.Katika mahojiano yake na gazeti la Kijerumani la “Bild am Sonntag”,waziri Steinmeier ametoa wito wa kuwaachilia huru wanamaji 15 wa Kingereza waliozuiliwa na Iran.Serikali mjini Teheran inawatuhumu wanamaji hao kuwa waliingia katika eneo la Iran.Uingereza lakini inasema wanamaji hao walikuwa katika eneo la Irak.