1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamburg kupiga kura ya maoni kuhusu Olimpiki

27 Novemba 2015

Ujerumani haijawahi kuandaa michezo hiyo tangu ile ya Munich 1972, na jaribio la karibuni lilizuiwa kupitia kura ya maoni Novemba 2013 iliyopinga ombi la Munich kuandaa Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya 2022

https://p.dw.com/p/1HDeo
Stimmzettel Olympia-Referendum Hamburg
Picha: Getty Images/Bongarts/A. Grimm

Maafisa wa Hamburg Kamati ya Michezo ya Olimpiki ya Ujerumani wanatumaini kupata wingi wa kura ili kuipiga jeki yao kuwasilisha ombi pamoja na miji ya Los Angeles, Pasris, Rome na Budapest ambapo uamuzi utafanywa na Kamati ya Kimataifa ya Olimpii – IOC kupitia uchaguzi wa mwaka wa 2017 wa mji utakaoandaa.

Nia ya Hamburg kuandaa michezo ya Olimpiki inaungwa mkono na vyama vingi vya kisiasa, chama cha wafanyabiashara wa mjini humo na vilabu vingi vya michezo, huku wanaopinga ombi hilo wakiwajumuisha wanaharakati wa mazingira na klabu ya divisheni ya pili ya St Pauli.

Utafiti unaonyesha kuwa wengi wanaunga mkono nia hiyo licha ya nyakati ngumu zilizopo kuhusiana na idadi kubwa ya wakimbizi na wahamiaji wanaoingia Ujerumani, wasiwasi wa usalama kutokana na mashambulizi ya Paris, na kashfa kadhaa katika ulimwengu wa michezo kuanzia kwa rushwa hadi matumizi ya dawa za kuongeza misuli nguvu.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/reuters
Mhariri: Josephat Charo