1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAMBURG : Wanne hawakuambukizwa sumu

12 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjz

Watu wanne waliohusishwa na suala la kupewa sumu kwa mpelelezi wa zamani wa Urusi Alexander Litvinenko wameonekana kuwa hawakumbukizwa na sumu hiyo.

Mpelelezi mkuu kutoka Shirika la Ujerumani la Kujilinda na Sumu ya Miale ya Nuklea Gerald Kirchner ameiambia radio ya Ujerumani kwamba watu hao wanne walifikishwa katika hospitali ya Hamburg kama hatua ya tahadhari.

Awali mtalaka wa Dmitry Kovtun na watoto wake wawili wadogo pamoja na mpenzi wake walionyesha ishara za kuambukizwa sumu hiyo.Kovtun,Andrei Lugovoi na Mrusi mwengine walikutana na Litvinenko katika hoteli ya London hapo tarehe Mosi Novemba.
Wiki tatu baadae Litvinenko alikufa kutokana na kima kikubwa cha sumu hiyo ya miale ya nunklea aina ya polonium 210 ambapo ishara zake zimeonekana kuwepo katika mji wa
Hamburg nchini Ujerumani.