1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamburg yapinga kuandaa michezo ya Olimpiki

Admin.WagnerD30 Novemba 2015

Wakaazi wa mji wa Hamburg wamekataa michezo ya olimpiki ya majira ya joto ya mwaka 2024 isifanyike katika mji wao baada ya kupiga kura ya maoni

https://p.dw.com/p/1HErt
Bürgerentscheid zu Olympia in Kiel und Hamburg Rote Ampel
Picha: picture-alliance/dpa/C. Rehder

Maafisa wa Ujerumani wanahofia kwamba hilo ni pigo kubwa kwa michezo hiyo nchini Ujerumani.

Hamburg ni mji wa hivi karibuni kabisa kutupilia mbali wazo la kutumia mabilioni ya dola kwa ajili ya michezo hiyo inayofanyika kwa muda wa siku 16 , ambapo kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC inaweka masharti na uwezekano wa faida unapatikana baada ya michezo hiyo.

Msemaji wa IOC amekiri kwamba , matokeo haya hayakuja kwa mshangao, lakini pia amesisitiza kwamba , "kwa uamuzi huo ni pigo kwa michezo nchini Ujerumani na mji huo."

Rais wa shirikisho la michezo ya olimpiki nchini Ujerumani DOSB Alfons Hoermann amesema kwamba "Ujerumani na wazo la Olimpiki haviendi pamoja kwa sasa" na ni lazima kutafuta njia mbadala kusaidia kuimarisha michezo nchini Ujerumani, wakati baraza la shirikisho hilo linatarajiwa kuketi siku ya Jumamosi wakati mchakato wa kutafuta nini kimetokea ukianza.

Gazeti la Sueddeutsche Zeitung limesema katika uhariri wake leo kwamba "wazo la Olimpiki nchini Ujerumani limezikwa kwa muda mrefu, baada ya wapiga kura asilimia 51.6 kukataa juhudi hizo, ikiwa ni wapiga kura asilimia 48.4 tu ndio waliokubali.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae /afpe / rtre
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman