1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HANOI: Rais George W.Bush awasili Vietnam kwa mkutano na nchi za Ashia na Pacific

17 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCrs

Rais wa Marekani, George W. Bush, amewasili katika mji mkuu wa Vietnam Hanoi, tayari kushiriki katika mkutano wa kilele wa nchi wanachama wa jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi kutoka Ashia na Pacific. Rais Bush ni rais wa pili wa Marekani kuwahi kuitembelea Vitennam tokea kumalizika vita vya Vietnam miongo mitatu iliopita. Mkutano huo ambao ni wa 21, unatazamiwa kuzungumzia zaidi uhusiano wa kibiashara. Kutakuwa pia na mazungumzo juu ya shughuli za kinyuklia za Korea ya kaskazini. Rais Bush atatafuta uungaji mkono wa pendekezo la nchi yake la kuweko eneo huru kibiashara. Waziri mkuu wa JapanShizo Abe na rais wa Uchina Hu Jintao ni miongoni mwa viongozi watakaohudhuria mkutano huo wa mjini Hanoi nchini Vietnam.