1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HANOI:Köhler ailaumu Vietnam kwa ukiukaji wa haki za binaadam

22 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzm

Rais Horst Köhler wa Ujerumani ameanza ziara yake nchini Vietnam kwa kupongeza ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.

Lakini hata hivyo Rais huyo wa Ujerumani aliilaumu Vietnam juu ya rikodi yake ya ukiukaji wa haki za binaadam na kwamba ulaya inasikitishwa na taarifa hiyo.

Rais Köhler alisema hayo baada ya mazungumzo yake na Rais Nguyen Mihn Triet wa Vietnam, ambayo pia yalijikita katika masuala ya elimu na mazingira.Ujerumani ni mshirika mkubwa kibiashara wa Vietnam, katika Umoja wa Ulaya.

Rais Köhler anaendelea na ziara yake ya wiki moja huko Asia kwa kuelekea China.