1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hanoi.mataifa ya APEC yaitaka Korea ya kaskazini kuachana na mpango wake wa kinuklia.

19 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCrP

Mataifa 21 ambayo yanaunda kundi la ushirikiano wa kiuchumi la mataifa ya Asia-Pacific yanasemekana kuwa yamekubaliana kimsingi kuhusu taarifa inayoitaka Korea ya kaskazini kuachana na mpango wake wa kinuklia.

Katika mkutano wao unaofanyika katika mji mkuu wa Vietnam Hanoi, viongozi wa mataifa ya kundi la APEC wanaripotiwa kuunga mkono waraka ambao unaelezea kuhusu azimio la hivi karibuni la baraza la usalama la umoja wa mataifa kuihusu Korea ya kaskazini.

Viongozi wanaohudhuria mkutano huo pia wameahidi kuanzisha upya kile kinachojulikana kama mazungumzo ya duru ya Doha ya biashara ambayo yamekwama tangu mwezi Julai.

Mataifa makubwa katika kundi hilo la APEC yanatarajiwa kupunguza ruzuku wanazotoa kwa wakuliwa wao pamoja na vipingamizi vya kibiashara vitaondolewa katika eneo hilo.

Mkutano huo wa siku mbili unahudhuriwa pia na marais kutoka Marekani, Russia na China.