1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hans-Dietrich Genscher atimiza miaka 80

Mohammed Abdul-Rahman21 Machi 2007

Ni miongoni mwa wanasiasa maarufu katika historia ya Ujerumani baada ya vita.

https://p.dw.com/p/CHlQ
Hans-Dietrich Genscher.
Hans-Dietrich Genscher.Picha: AP

Hans -Dietrich Genscher aliivaa kofia ya kisiasa na hadi leo hakuna aliyekua maarufu hadi leo katika wadhiafa aliyoushikilia na hasa katika wizara ya amambo ya nchi za nje kama Genscher . Alianzia kama waziri wa ndani katika serikali ya Kansela Willy Brandt 1969 hadi 1974. Wengine wakimwita kwa utani “ mtu mwenye fulana ya manjano”- akipendelea sana kujitambulisha kwa rangi za chama chake cha FDP-buluu na majano-Genscher akageuka mwanadiplomasia, akisafiri huku na kule kama Waziri wa mambo ya nchi za nje.

Mwaka 1977 akaizuru Beijing mara abaada ya kifo cha Mwenyekiti Mao Zedong. Baada ya Warusi kuingia na kuivamia Afghanistan mwishoni mwa 1979, alitoa wito wa msimamo mkali dhidi ya Urusi. Akiwa ni mstahamilivu Genscher alizusha maajabu katika safu ya kisiasa. Alipokwenda Mosko kukutana na Kiongozi na kiongozi wa Urusi Mikhail Gorbachov 1985, aliweza kutumia vyema nafasi hiyo kufafanua kwa uwazi msimamo wa Ujerumani.

Wakati wa mabadiliko ya kusisimua katika Ujerumani mashariki ya zamani kutokana na kuanguka ukuta wa Berlin, msimu wa kiangazi 1989, kutoka kwenye veranda ya ghorofa ya jingo la ubalozi wa Ujerumani mjini Prag, mbele ya maelfu ya wajerumani mashariki waliokimbilia humo, akawatangazia uamuzi wa kuwapa kibali cha kusafiri hadi Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, akisema “Tumekuja kwenu , ili kushirikiana nanyi na kwamba leo mnapata kibali cha kusafiri nje.”

Kwake Genscher kuungana tena kwa Ujerumani ilikaua kama ndoto. Hapa Genscher aliyezaliwa Ujerumani mashariki ya zamani alipigwa na mshangao alipotunzwa shahada ya udaktari wa heshima na chuo kikuu cha Leipzig na kutamka ,“Ninawashukuru kwa tunzo hii na ninaipokea kwa moyo mkunjufu Shahada hii ya udaktari wa heshima kutoka kitivo cha sheria hapa Liepzig, na kama nina ruhusa ya kutamka ni kitivo changu nikikumbuka 1948.”

Hans Dietrich Genscher alizaliwa Halle 1927. baada aya elimu ya sekondari alisoma sheria. Akiwa mwanachama wa chama cha Liberal Democrat cha Ujerumani aliishi kwanza katika Ujerumani ya kikoministi ya DDR. 1952 akahamia Bremen na huko akajikita katika chama cha FDP. Akiwa mwanasheria kijana alipanda haraka. 1965 akachaguliwa kwa mara ya kwanza mbunge wa bunge la Ujerumani-Bundestag .

Alipokua waziri wa ndani, mtihani wake mkubwa ni tukio la 1972 wakati wa michezo ya olimpiki, pale magaidi wakiarabu walipoawateka nyara wanamichezo wa Kiisraili mjini Munich na kuwauwa .Barua yake kutaka kujiuzulu ilikataliwa na Kansela Willy Brandt.

Alipojiuzulu Brandt binafsi kwa kutokana na kashfa ya ujasusi iliomhusisha msaidizi wake wa karibu, Genscher akawa Waziri mpya wa mambo ya nchi za nje akichukua naafasi ya mtangulizi wake Walter Scheel , wakati huo huo akishika uongozi wa chama cha FDP, alichokiongoza kwa miaka 11.

Kufuatia mabadiliko ya serikali, FDP ikaachana na muungano na Social democrats-SPD chini ya Helmut Schmidt –SPD na kujiunga na Christian Democratic Union –CDU ilioongozwa na Helmut Kohl kuunda serikali mpya ya mseto. Hatua hiyo ilizusha misuko suko mingi katika FDP. Karibu miaka 10 baadae, Mei 1992, Genscher akauacha wadhifa wake kama Waziri wa mambo ya nchi za nje na kustaafu.