1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harakati za kiusalama kuwekwa nchini Kenya dhidi ya kundi la Al Shabab

20 Oktoba 2011

Rais wa Kenya Mwai kibaki hii leo amesema serikali yake itafanya kila mbinu ya kuilinda nchi pamoja na raia wake.

https://p.dw.com/p/12vmz
***Für mögliche Ergänzungen der Karte, wie z.B. andere Sprachen, zusätzliche Orte oder Markierungskreuz, wenden Sie sich bitte an infografik@dw-world.de (-2566), Außerhalb der Bürozeiten an bilder@dw-world.de (-2555).*** DW-Grafik: Per Sander 2011_03_10_Laender_Prio_A_B
Majeshi ya Kenya tayari kwa mapambano nchini humoPicha: dapd

Rais Kibaki amesema juhudi hizo zinafanyika ili kuhakikisha kuwa Kenya inaendelea kuwa na uthabiti na amani.

Hayo ni matamshi ya kwanza ya rais wa Kenya tangt vikosi vya kijeshi kuingia Somalia katika juhudi za kupambana na kundi la waasi la Al Shabab, linaloaaminika kutekeleza visa tofauti vya utekaji nyara nchini humo.

Huku hayo yakiarifiwa, sasa Kenya inatarajiwa kuanzisha msako mkubwa nchini humo wa kuendelea kuwasaka waasi wa kundi hilo.

Naibu waziri wa usalama wa ndani Orwa Ojode, amesema operesheni hiyo itakayokuwa kubwa zaidi kuwahi kutokea mjini Nairobi itafanyika katika kitongoji cha Eastleigh, mashariki mwa mji. Eastleigh ni eneo linaloojulikana kama Somalia ndogo kwa kuwa na idadi kubwa ya Wasomali wanaoishi huko.

Akitangaza harakati za operesheni hiyo bungeni hapo jana, bwana Ojode alisema vita dhidi ya Al Shabab ni kama mnyama mkubwa ambaye mkia wake uko nchini Somalia na kichwa chake kiko Kenya hasa upande wa Eastleigh.

Flash-Galerie UNHCR 60 Jahre Auswahl 1
Recently-arrived Somali refugees wait to be registered at a reception center at Dagahaley Camp, outside Dadaab, Kenya, Sunday, July 10, 2011. UNHCR estimates 1300 new refugees fleeing drought and hunger in Somalia are arriving daily in the Dadaab area of northern Kenya. (AP Photo/Rebecca Blackwell)Picha: AP

Hata hivyo habari ya operesheni hiyo haikupokelewa vyema na baadhi ya wabunge waliotoka kaskazini mwa Kenya. Wabunge hao walisema kuwa wanaunga mkono moja kwa moja harakati za kusaka kundi la waasi la Al Shabab, lakini wakamshutumu bwana Ojode na kusema hatua hiyo inawatenga Wasomali raia wa Kenya walioko nchini humo.

Kwa upande wake bwana Ojode amesema hatasimamisha operesheni hizo kwa sababu katiba ya Kenya inashinikiza serikali kuwalinda raia wake, na kuwa hiyo ni moja ya harakati ya serikali ya Kenya kufanya hivyo.

Miongoni mwa wabunge wanaopinga pendekezo hilo ni Adan Keynan mbunge wa Wajir Magharibi, mbunge mteule Mohammed Affey na mbunge wa Dujis Adan Dualle, waliosema kuwa Wasomali raia wa Kenya wanapaswa kulindwa na pendekezo la Orwa Ojode litakuwa ni kinyume na vile katiba ya Kenya inavyosema, kuwa kila Mkenya ana haki ya kulindwa na serikali.

Katika mikakati hiyo ya kiusalama ambayo bado haijulikani ni lini itaanza, wanaotumia usafiri wa angani na ardhini watakaguliwa watakopokuwa wakielekea na kutoka katika maeneo yanayopakana na Somalia.

Tangu harakati za kijeshi za kuwasaka al Shabab maarufu kama "Operesheni Linda Nchi" kuanza siku tano zilizopita, ulinzi umeimarishwa katika maeneo muhimu nchini Kenya kama vile vituo vya usafiri, mahoteli, maeneo ya watu wengi na sehemu za watalii.

Hata hivyo wadadisi wa masuala ya usalama wanasema, mikakati inayopangwa kufanyika mjini Nairobi haitakuwa rahisi, kwani ni vigumu kutofautisha Wasomali kutoka Kenya na wale wa Somalia.

Muandishi Amina Abubakar/AFPE

Mhariri Josephat Charo.