1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE: Polisi wazima mkutano wa hadhara

19 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQp

Polisi nchini Zimbabwe walifaulu jana kuzuia mkutano wa hadhara uliotishwa na chama kikuu cha upinzani, Movement for Democratic Change, MDC, mjini Harare.

Kiongozi wa chama hicho, Morgan Tsvangirai, alipania kuutumia mkutano huo kuanzisha kampeni yake ya kuwania wadhifa wa urais nchini Zimbabwe.

Uchaguzi wa rais nchini humo unatakiwa kufanyika mwaka ujao lakini rais Robert Mugabe anataka kuuahirisha hadi mwaka wa 2010.

Chama tawala nchini Zimbabwe, ZANU PF, kimeuunga mkono mpango wa rais Mugabe lakini unahitaji kuidhinishwa na bunge.