1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE : Wazalendo kupatiwa hisa kubwa ya kiuchumi

17 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1A

Baraza la mawaziri la Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe limepitisha mswada wa sheria wenye lengo la kuwapatia asilimia 51 ya hisa katika makampuni wazalendo wa Zimbabwe.

Waziri wa Uzawa na Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi Paul Mangwana amesema katika matamshi yaliokaririwa na gazeti la serikali la Herald kwamba muswada huo sasa utawasilishwa bungeni kuzingatiwa.

Kwa mujibu wa gazeti hilo la Herald iwapo muswada huo utapita serikali itatumia sheria hiyo mpya kuendeleza kuwapa uwezo wa kiuchumi wananchi kwa kutenga asilimia 51 ya hisa katika uchumi kwa wazalendo asilia wa Zimbabwe.

Muswada huo yumkini ukaleta hofu kwa takriban kampuni zote za kigeni au zile zinazomilikiwa na wazungu zilioko kwenye sekta ya madini,utalii na uzalishaji viwandani.