HARARE:Twiga anusurika
22 Septemba 2007Matangazo
Polisi nchini Zimbabwe waliwazuia wanakijiji kumchinja na kumla twiga mmoja aliyepoteza njia mjini Harare.Twiga huyo aliyekuwa pekee anaaminika kuingia mkoa wa kusini wa Seke kutoka shamba moja lililokuwa karibu.Uongozi wa mbuga za wanyama ulimuondoa twiga huyo baada ya polisi kuzuia umati wa watu kumuua na kumpika.Zimbabwe inakabiliwa na uhaba mkubwa wa nyama na bidhaa za matumizi kufuatia mkwamo wa kiuchumi na mfumko wa bei uliofikia takriban asilimia alfu 7.