1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE:Visa vya Malaria vyapungua

19 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHS

Visa vya malaria nchini Zimbabwe vimepungua kutoka milioni 3 hadi milioni 1.8 katika kipindi cha mwaka uliopita kwa mujibu wa gazeti la serikali la The Herald.

Kulingana na Portia Manangazira afisa wa ngazi za juu katika Wizara ya Afya,nchi hiyo imeimarisha hatua za kukabiliana na ugonjwa wa malaria unaosababisha vifo vingi nchini Zimbabwe.

Hatua hizo zinajumuisha unyunyizaji wa dawa katika maeneo yaliyo na mbu,kampeni za uhamasishaji vilevile kusambaza vyandarua vya mbu katika maeneo yaliyoathirika.Hata hivyo hali hiyo ingeimarika zaidi endapo Zimbabwe ingepata ufadhili kwa wakati mwafaka kutoka kwa Mfuko wa Fedha Duniani Global Fund.

Kwa mujibu wa Bi Manangazira sera mpya ya kukabiliana na malaria inajumuisha utumiaji wa aina mpya ya dawa za kutibu malaria.Kiongozi huyo anaongeza kuwa nchi yake ina dawa za kutosha za akiba kwa sasa.Asilimia 40 ya watu ulimwenguni wanakabiliwa na hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa malaria unaosababisha vifo vya watu alfu nne u nusu kila siku wengi wao wakiwa watoto walio chini ya miaka mitano.