1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE:Wafuasi wa MDC waachiwa

8 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtd

Wafuasi 11 wa upinzani nchini Zimbabwe waliokuwa wamezuiliwa kwa miezi miwili wameachiwa huru.Watu hao waliokamatwa kwa madai ya kuunda njama ya ugaidi waliachiwa baada ya mahakama kufuta madai yanayowakabili kwa mujibu wa msemaji wa chama cha MDC Nelson Chamisa.

Watu hao 11 wakiwemo wafanyikazi 7 wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change, MDC walikamatwa katika msako mwezi Machi pale polisi walipodai kuwa walivunja njama ya kurusha mabomu ya petroli.Wengine 20 waliokamatwa wakati huohuo bado wanazuiliwa akiwemo mbunge wa chama hicho Paul Madzore.

Bwana Madzore na wengine 30 walikamatwa siku kadhaa baada maafisa wa uasalama kumpiga vibaya kiongozi wa MDC Morgan Tsvangirai pamoja na wafuasi wake katika maandamano ya kumpinga Rais Robert Mugabe