1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE:Zaidi ya watu 1300 kwa kukiuka amri ya serikali ya kuwataka wapunguze bei za bidhaa

10 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkM

Zaidi ya watu 1300 nchini Zimbabwe wanaomiliki maduka na wakuu wa biashara wamekatwa na wengine kutozwa faini kwa kukiuka amri ya serikali ya kupunguza bei.

Kwa mujibu wa radio ya Taifa wakuu wa kampuni 33 ni miongoni wa wale waliokamatwa tangu ijumaa iliyopita na wanatazamiwa kufikishwa mahakamani.

Serikali ya rais Mugabe iliagiza bei za bidhaa na huduma mbali mbali kupunguzwa nusu ili kukabiliana na mfumko wa bei ambao umefikia zaidi ya asilimia 3700.

Hata hivyo wafanyibiashara wanalalamika kwamba bei ya bidhaa iliyotolewa na serikali inawafanya wasiweze kumudu kulipia gharama ya biashara zao.

Wengi wa wafanyibiashara nchini humo wamelazimika kufunga na kusababisha kuenea kwa upungufu mkubwa wa bidhaa muhimu kama vile mafuta ya kupikia na chumvi.