1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE:Zimbabwe yatangaza sheria mpya kudhibiti mashirika ya misaada

28 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6A

Zimbabwe leo imetangaza sheria mpya za udhibiti wa mashirika ya misaada na mashirika yasiyoya kiserikali.

Mashirika hayo ni pamoja na makundi ya kutetea demokrasia nay ale ya haki za binadamu ambayo serikali ya Mugabe inasema yanaendesha kampeini dhidi yake.

Sheria hiyo mpya inayataka mashirika hayo kuomba leseni kutoka kwa serikali ambapo yanaweza kunyimwa au kuyazuia kuendesha shughuli zao.

Utaratibu huo wa sheria mpya umetangazwa kwenye maandiko rasmi ya serikali kufuatia onyo lililotolewa hivi karibuni na maafisa wa serikali dhidi ya mashirika ya misaada yanayojiingiza katika masuala ya kisiasa.Serikali ya Zimbabwe inadai baadhi ya mashirika ya misaada yanaleta misaada ya chakula Zimbabwe halafu yanajitumbukiza kwenye mambo yasiyowahusu ya kutaka mageuzi ya utawala.