1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harry Kane aendelea kutamba Ujerumani

29 Januari 2024

Harry Kane alifunga bao lake la 23 msimu huu wakati Bayern ikipata ushindi muhimu wa 3-2 dhidi ya Augsburg na kupunguza mwanya na Leverkusen katika mbio za kuwania ubingwa.

https://p.dw.com/p/4bner
Bundesliga ; Augsburg  dhidi ya Bayern Munich
Mshambuliaji Harrya Kane akipambana na Jeffrey Gouweleeuw wa Augsburg katika mechi ya mzunguko wa 19 Bundesliga.Picha: Sven Hoppe/dpa/picture alliance

Augsburg waliingia kwenye mchezo huu wakiwa wameshinda mechi zao mbili za awali za nyumbani dhidi ya Bayern, na walianza kwa kujiamini kutafuta ushindi wa tatu lakini maji yalizidi unga.

Vinara wa Bundesliga, Bayer Leverkusen walipoteza nafasi nyingi kabla ya kulazimishwa sare ya 0-0 dhidi ya wageni Borussia Moenchengladbach na kusababisha uongozi wao kileleni kipungua hadi pointi mbili.

Leverkusen imeanza kusuasua 

Bayer Leverkusen
Kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso akifuatilia mechi Picha: Marius Becker/dpa/picture alliance

Kocha wa Leverkusen Xabi Alonso alisema matokeo waliyopata siyo waliyoyataka lakini wataendelea kujitahidi.

Soma pia: Harry Kane amaliza ukame wa mabao kwa kuipa ushindi Bayern Munich dhidi ya Stuttgart

"Tutashughulikia vizuri. Hakuna jipya kwenye soka. Tunajua kuwa aina hii ya michezo hufanyika, unatengeneza nafasi nyingi lakini unashindwa katika umaliziaji haikukusudiwa iwe hivyo. Tulifanya kila mbinu lakini kwenye eneo la kisanduku?? hatukufanikiwa  kufunga bao, jambo ambalo kwa matumaini lingetupa ladha ya kuendelea kucheza. Unapaswa pia kuheshimu jinsi walivyojilinda . Walifanya vizuri sana. Ilikuwa ngumu kwetu kupata nafasi nzuri za kufunga bao.” Alisema Alonso.

Katika mechi nyengine, Deniz Undav alitia kimyani hat-trick yake ya kwanza ya Bundesliga wakati Stuttgart walipoicharaza  Leipzig mabao 5-2  na kutilia mkazo azma yao ya kutinga hatua ya nne-bora.

Borussia Dortmund imerudia kasi yake ya ushindi kwa kuilaza Bochum 3-1, ushindi wa tatu mfulilizo mwaka huu na kupanda hadi nafasi ya nne kwa pointi 36.

Eintracht Frankfurt iliangukia bao 1-0 dhidi ya Mainz.  Marvin Ducksch and Justin Njinmah walifanya kazi ya ziada kwa kufanikisha ushindi wa 3-1 ugenini dhidi ya Freiburg. Hoffeinheim ilitoka sare ya 1-1 na Heideinhem. huku FC Cologne ikiendelea kujaribu kujiondoa mkiani kwa kuandikisha sare ya 1-1 dhidi ya Wolfburg.

Soma pia: FC Cologne waondoka kwa muda kutoka eneo la kushushwa daraja

Marie-Louise Eta aliweka historia siku ya Jumapili kwa kuwa kocha wa kwanza wa kike kuchukua jukumu la kusimamia mechi ya Bundesliga, na kuiongoza Union Berlin kushinda Darmstadt bao moja kwa bila. Eta alichukua jukumu la kuinoa timu hiyo katika mechi ya nyumbani baada ya kocha Nenad Bjelica kusimamishwa kazi.