1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIndia

Ndoa za dini tofauti zaendelea kuzusha wasiwasi India

13 Januari 2023

Ndoa za dini tofauti nchini India zinaendelea kuzusha wasiwasi nchini India. Makundi yanayopinga watu kubadili dini kwa ajili ya kufunga ndoa kati ya wahindu na Waislamu wanakabiliwa na vitisho na kuuawa.

https://p.dw.com/p/4M73p
Indien Kultur Religion l Traditionelle Hochzeit, Braut in Mumbai
Picha: Fariha Farooqui/Xinhua/picture alliance

Katika kisa kimoja miaka miwili iliyopita, polisi wa India walisimamisha ndoa ya dini tofauti licha ya idhini ya familia zote mbili. Kabla ya harusi kuanza, polisi waliingilia kati baada ya kiongozi wa eneo la watu wenye kuegemea mrengo wa kulia wa wahindu kutoa malalamiko. Soma : India kuondoa baadhi ya vikwazo Kashmir

Nchini India, ndoa nyingi bado hupangwa na familia. Ndoa za watu wa madhehebu na dini tofauti zinadharauliwa na kuchukuliwa kuwa ni mwiko katika sehemu nyingi.

Katika matukio mabaya zaidi, familia zimeshambuliwa au hata kuuwawa kwa wanandoa kwa sababu ya kupendana au kwa kujaribu kuoa mtu ambaye si dini yao.

Takriban majimbo manane, yakiwemo sita yanayotawaliwa na chama tawala cha Hindu Bharatiya Janata Party (BJP), yamepitisha sheria za kupinga uongofu ambazo zinapiga marufuku kubadilisha dini kwa madhumuni ya ndoa pekee.

Indien spirituelle Hochzeit in Goa
Wanandoa wa ulaya wakiwa katika mavazi ya ndoa za IndiaPicha: Vicki Couchman/Design Pics/picture alliance

Mwezi uliopita, katika jimbo la magharibi la Maharashtra, serikali iliunda jopo la watu 13 kuchunguza ndoa za dini tofauti katika jimbo hilo na kudumisha rekodi ya wanandoa na familia zao.

Kikundi cha Wahindi wenye msimamo mkali,cha Vishva Hindu Parishad (VHP),mwezi uliopita kilizindua "kampeni ya uhamasishaji" umma nchini kote, wakidai kuwa wanawake wa Kihindi wanashikiliwa katika kile walichokitaja kama "jihadi ya mapenzi " na mazungumzo ya kidini yanayokwenda kinyume cha sheria.

"Jihadi ya mapenzi " ni neno la dharau linalotumiwa na Wahindi wa mrengo wa kulia kuelezea jambo linalodaiwa kuwa wanaume wa Kiislamu huwarubuni wanawake wa Kihindi kwenye ndoa na kusilimu huku vikundi vya Kihindi vikinadai, bila ushahidi kuwa ni njama iliyopangwa.

Asif Iqbal, mwanzilishi mwenza wa shirika lisilo la kiserekali la "Dhanak of Humanity," jukwaa la kutoa msaada kwa wanandoa wa dini tofauti, aliiambia DW kwamba wanandoa wengi wanaishi kwa hofu ya mahusiano yao kuwa kosa la jinai chini ya majaribio ya sasa ya marekebisho ya kisheria.

Katika muongo moja uliopita, shirika hilo limesaidia zaidi ya wanandoa 5,000 wa imani, matabaka na jumuiya mbalimbali kuja pamoja. Hata hivyo, Iqbal alisema idadi ya wanandoa wanaokuja kutafuta msaada imepungua kwa kasi.

Indien Kultur Religion l Traditionelle Hochzeit, Trans
Wanandoa huko IndiaPicha: Satyajit Shaw/Pacific Press/picture alliance

Huku kukiwa na mivutano ya kijumuiya katika miaka ya hivi majuzi, wanandoa wa dini na matabaka tofauti nchini India wanakabiliwa na uonevu, unyanyasaji, upinzani kutoka kwa jamaa zao na hata vitisho vya kuuawa.

Tangu chama cha BJP kilipochaguliwa mwaka wa 2014, mvutano kati ya Wahindi na Waislamu umezidi kuwa na mgawanyiko. Kuanzishwa kwa sheria za kupinga uongofu ni dalili ya kuongezeka kwa utaifa wa Kihindu, wanasema wanaharakati.

Mwanasheria anayezingatia sheria ya familia na mali Malavika Rajkotia, ameiambia DW kwamba sheria ni mbinu ya vitisho dhidi ya jamii za walio wachache. Sasa, hata usajili maalum wa sheria za ndoa, kwa ndoa za dini tofauti ni msingi wa unyanyasaji kwa vijana.

Sheria maalum ya ndoa nchini India ilipitishwa ili kuhalalisha na kusajili ndoa za kidini na tabaka na kuruhusu watu wazima wawili kuoana kupitia mkataba wa kiraia. Hata hivyo, wanandoa wanapaswa kungoja kwa zaidi ya mwezi mmoja ili kusajili ndoa yao, hatua inayotoa nafasi kwa wakati wa kunyanyaswa na familia na mamlaka wasiokubali.

Kulingana na Katiba ya India, raia wana uhuru wa "kukiri, kutekeleza na kueneza" dini. Neno "kueneza" pia linajumuisha haki ya raia kubadili dini.