1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatari ugonjwa wa kifua kikuu kutanda katika Ulaya ya magharibi

10 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4C

Shirika la afya duniani, WHO, limeonya kwamba bara la Ulaya linakabiliwa na kitisho kikubwa cha ugonjwa wa kifua kikuu tangu vita vikuu vya pili vya dunia. Shirika hilo linasema ugonjwa huo wa kifua kikuu umeanza kuwa sugu kwa madawa. Na miongoni mwa nchi 20 ugonjwa huo ni sugu, 14 zinapatikana katika maeneo ya Ulaya ya mashariki na Ashia ya kati.

Shirika la WHO na mashirika mengine 20 ya afya, yameonya kuwa huenda ugonjwa huo ukatanda katika eneo la Ulaya ya magharibi ikiwa hazitachukuliwa hatua madhubuti mapema iwezekanavyo.

Kiasi ya watu nusu milioni huambukizwa kifua kikuu barani Ulaya na Ashia kila mwaka ambapo 70,000 miongoni hao hufariki dunia kutokana na ugonjwa huo ambao unawauwa watu 5,000 kila siku duniani.