1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hati za siri za Marekani zafichuliwa

10 Juni 2013

Visa vya kuchunguzwa mawasiliano ya simu ndani na nje ya Marekani vinaikumba nchi hiyo na idara zake za upelelezi.Wizara ya ulinzi imethibitisha uchunguzi wa kupatiwa vyombo vya habari mpango wa siri kunasa mawasiliano

https://p.dw.com/p/18mjs
Mtumishi wa zamani wa shirika la Upelelezi la Marekani CIA Edward SnowdenPicha: Reuters/Ewen MacAskill/The Guardian/Handout

Edward Snowden,mtumishi wa zamani wa shirika la upelelezi la Marekani,CIA amefichua kuwa chanzo cha kuvuja mipango ya upelelezi unaofanywa na idara ya ujasusi ya Marekani.Ameyapatia magazeti ya Guardian la Uingereza na Washington Post la Marekani nyaraka zinazothibitisha kuwepo mpango wa siri wa ukaguzi kwa jina PRISM unaoruhsu kuwachunguza wamarekani.Edward Snowden anasema amefanya hivyo kwasababu ya umuhimu wa "kulinda haki za kimsingi."

Magazeti ya Guardian na Washington Post yamechapisha wiki iliyopita habari za siri kutoka taasisi ya usalama wa taifa.Habari hizo zinaeleza jinsi taasisi hiyo ambayo ni mojawapo ya taasisi muhimu za upelelezi za Marekani ilivyonasa mawasiliano ya simu na kupitia mtandao kwa mfano wa Verizon,Google,Apple na mtandao wa kijamii wa Facebook.Muda mfupi kabla ya ripoti hizo kufichuliwa Edward Snowden amekimbilia Hong Kong.Katika mahojiano pamoja na gazeti la Guardian,kijana huyo mwenye umri wa miaka 29 amesema amekimbilia katika hoteli moja ya Hong Kong.Ameitaja misingi madhubuti ya uhuru wa mtu kutoa maoni yake inayoheshimiwa Hong Kong na kusema anataraji viongozi wa serikali katika eneo hilo la kusini mwa China,hawatamrejesha Marekani ambako anakabiliwa na hatari ya kufikishwa mahakamani.

Snowden anataka kwenda Island

Symbolbild USA Geheimdienst Überwachung
Mojawapo ya mbinu za upelelezi za MarekaniPicha: Fotolia/benjaminnolte

Ikulu ya Marekani na shirika la upelelezi la CIA hawakusema chochote kuhusu kadhia hiyo ya Snowden.Shawn Turner,msemaji wa mkurugenzi wa upelelezi wa taifa DNI anaesimamia shughuli za mashirika tofauti ya upelelezi ya Marekani,amekumbusha tu,tunanukuu "mtu yeyote anaehusika na masuala ya usalama anatambua kwamba ana jukumu la kuhifadhi habari zilizotengwa na kuheshimu sheria."

Edward Snowden anapanga kukimbilia Island nchi inayosifiwa kuwa mshika bendera wa nchi zinazotetea uhuru wa maoni katika mtandao.

Kufichuliwa mpango huo wa PRISM kumezusha mjadala mkali nchini Marekani na kwengineko ulimwenguni kuhusu madaraka makubwa ya shirika la usalama wa taifa NSA.Tangu september 11 mwaka 2001 taasisi hiyo imepanua miradi yake ya upelelezi,ingawa viongozi wa Marekani wanahoji miradi hiyo inaambatana na sheria.

Kenya ni miongoni mwa nchi ambako mawasiliano ya mtandao yanasikilizwa

USA Hauptquartier NSA Fort Meade
Makao makuu ya shirika la usalama wa taifa-NSA huko Fort MeadePicha: Getty Images

Mashirika ya upelelezi ya Marekani yanapeleleza katika sehemu nyengine pia za dunia.Katika eneo la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara,Kenya imeorodheshwa kama nchi inayokamata nafasi ya mbele kabisa miongoni mwa nchi ambako mawasiliano ya simu na mtandao yananaswa.Kenya imeorodhweshwa katika eneo la rangi ya manjano pamoja na Saud Arabia,Jordan,Ujerumani.

Mwandisahi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/AFP

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman