1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hati za umiliki husaidia kupunguza migogoro

23 Agosti 2016

Nchini Tanzania kumekuwa na mzozo mkubwa wa matumizi ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji. Lakini juhudi za hivi karibuni za kutoa hati za umiliki wa ardhi zinaanza kutoa matunda katika kupunguza mizozo hiyo.

https://p.dw.com/p/1Jnkl
Mfugaji wa kimasai ambaye anaishi mpakani mwa Kenya na TanzaniaPicha: picture-alliance/Ton Koene

Hali hii inaelezwa kuchangiwa na uandikishaji duni wa umiliki wa ardhi ambao kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na shirika uwazi la kimataifa yaani Transparency International 2014 Global Corruption mchakato wa upimaji nchini humo meghubikwa na rushwa.

Udhaifu huo umezidi kusababisha migororo ambayo inalipelekea shirika la hisani la kimataifa la Farm Afrika Tanzania kwa kushirikiana na mabaraza ya vijini kuanzisha mradi wa upimaji ardhi katika wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara kaskazini mwa nchi hiyo, ambao una lengo la kupanga matumizi sahihi ya ardhi na kupunguza migogoro.

Wakati wakulima wengi nchini humo wanatumia ardhi kuendesha kilimo cha mazao mbalimbali, bado hawana uthibitisho wa kuonyesha kuwa wanamiliki maeneo hayo kihalali hali inayowaweka wamiliki wengi katika hali ya wasiwaasi.

Hali ambayo imewapa nafsi watu wengi hasa wenye uwezo kuvamia na kuchukua ardhi ambayo si yao.

Katrina Hhaynahhi na mumewe Saimon ni miongoni mwa Watanzania wengi ambao wameathiriwa na migogogro ya ardhi.

Kwa miaka minne wameishi katika mgogoro wa matumizi ya ardhi na jirani yao ambaye amekuwa akilisha mifugo yake katika eneo ambalo lao ambalo wao hulitumia kwa ajili ya kilimo.

farmer shows her dry maize field, Tanzania
Mkulima wa mahindi Mkoani Morogoro nchini TanzaniaPicha: CC/ CIMMYT

Mradi wa upimaji maeneo na kutoa hati za umiliki kimila unaotekelezwa na shirika hilo unaleta amani tena kwao ambapo sasa eneo lao limepimwa na kupatiwa hati ya umiliki ardhi ambayo inawapa mamlaka ya kisheria kumiliki eneo hilo lanye ukubwa wa hekari 11.

Katrina anasema na hapa ninamnukuu:

"Hati hii inamaanisha kitu kikubwa sana kwetu, eneo letu sasa liko salama hatutegemei mogogoro tena na jirani zetu." Mwisho wa kumnukuu

Hati hii inawapa uhakika wa kuwekeza zaidi katika kilimo katika eneo hilo ili kujiongezea kipato cha familia.

Hati za umiliki wa ardhi husaidia matumizi bora ya rasilimali

Meneja wa Farm Afrika Tanzania, Beartice Maliahela, anasema kuhakiki umiliki wa ardhi hasa maeneo ya vijijini ni wa muhimu kwa sababu unasaidia kuziwezesha jamii za watu waishio huko kuwa na haki ya kumiliki na kulinda ardhi pamoja na rasilimali zake.

Kwa mujibu wa Maliahela tangu shirika lake lianzishe mradi huo miaka miwili iliyopita wamesaidia kutatuta migogoro ya ardhi hasa inayotokana na kuongeza maeneo ya kilimo na unyweshaji wa mifugo.

Sheria ya ardhi ya vijiji nchini Tanzania ya mwaka 1999 inayapa mamlaka mabaraza ya vijiji kufanya maamuzi ya matumizi ya ardhi ambapo katika mradi huu Farm Afrika inashirikiana na mabaraza hayo.

Mwandishi: Celina Mwakabwale/Reuters
Mhariri: Mohammed Khelef