1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatima ya chelsea na kocha wake scolari ?

15 Januari 2009

Na je,Podolski anarejea FC Cologne ?

https://p.dw.com/p/GZ4z
Lukas PodolskiPicha: picture-alliance/ dpa

Kufuatia pigo la mwishoni mwa wiki la mabao 3 bila majibu iliopata Chelsea kutoka mabingwa Manchester united katika premier League,hatima ya Chelsea msimu huu na kocha wake mbrazil Luiz Scolari imo mashakani.Manchester City haikukata bado tamaa kumuajiri stadi wa Brazil Kaka.Na FC Cologne,inasema kufuatia majadiliano ya jana mjini munich, stadi wao wa zamani Lukas Podolski yuko njiani kurejea Cologne mwishoni mwa msimu huu. Nae aliekua nahodha wa Ufaransa, Patrick Vieri anazingatia kutundika buti kwa timu ya Taifa.

Eric Ponda asimulia :

Ule mchezo wa kamari wa wiki kadhaa sasa kati ya mabingwa Bayern Munich na FC Cologne juu ya hatima ya Lukas Podolski, ama kurejea kuichezea Cologne au kubakia Munich sasa inakaribia kumalizik.Kufuatia mazungumzo ya juzi huko Munich, FC Cologne imetangaza kuwa iliobaki sasa ni kutiwa saini tu mkataba,lakini wajumbe wamerudi kutoka Munich wameridhika.

Podoslki,stadi wa timu ya Taifa, amekuwa haridhiki na Bayern Munich kwavile nadra kuchezeshwa kuanzia mwanzo . Mara nyingi akiwekwa akiba tu.

Kinyume na FC Cologne, huko kabla kujiunga na Munich 2006, pale Cologne ilipozama daraja ya pili,Podolski alikuwa ni nyota inayonawiri.Sasa inaonesha ni swali la wakati lini-mwanamfalme Podolski kama wanavyomuita mashabiki wa Cologne atarudi nyumbani maskani mwake.

Huko Ufaransa, taarifa zasema mshambulizi wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa Sylvain wiltord anakaribia kufunga mkataba na Olympique Marseille akiazimwa tu kwa miezi 6 kutoka Stade Rennes.

Wiltord mwenye umri wa miaka 34 ,ametia mabao 26 kwa kuichezea Ufaransa mara 92 kati ya 1999 na 2006.Nae nahodha wa zamani patrick Vieira amesema anazingatia kuacha kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa.

Meneja wa Manchester City,Mark Hughes aliarifu jana kuwa mpango wa kumuajiri stadi wa Brazil Kaka kutoka AC Milan ya Itali bado upo pale pale.Hapo kabla taarifa kutoka Falme za nchi za kiarabu-Emirates-ambako ndiko waliko matajiri wa Manchester City,mradi wa kumuajiri kaka umevunjika kufuatia mazungumzo kati ya AC Milan na Manchester City.

Mark Hughes anashikilia lakini mpango huo bado haujavunjika.

ripoti za vyombo vya habari zilisema kwamba Manchester city ilikuwa tayari kutoa kitita kikubwa kabisa cha hadi Euro milioni 100 sawa na dala milioni 132 kumkomboa Kaka kutoka AC Milan.

Kaka mwenyewe amesema anafurahia kubakia Milan.

Wakati Manchester City inamlilia Kaka kujiimarisha katika Premier League, Chelsea ambayo hadi juzi ikisimama nafasi ya pili nyuma ya viongozi wa Ligi-Liverpool, haijui hatima yake wala ya kocha wake mbrazil Felipe Scolari.Manchester United imeshaipiku Chelsea na inanyatia taji la ubingwa wa uingereza sasa kutoka nafasi ya pili.

Ingawa mabingwa wengi hawaamini kuwa wakati huu kocha huyo wa Brazil alieiongoza kutwaa kombe la dunia ataiacha mkono Chelsea,kuna mengi anayopasa kurekebisha katika kikosi chake.

Scolari amekuwa kocha nchini Brazil,Kuweit,Saudi Arabia na Ureno kwa muda wa miaka 25 kabla hakushika hatamu za Chelsea katika premier League.hii ilifuatia kutimuliwa kwa mreno Jose Mourinho.Kwa sasa lakini ni mapema kusema Scolari ataihama Chelsea.