1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatima ya Ugiriki baada ya makubaliano ya Brussels

Oumilkher Hamidou22 Februari 2012

Makubaliano ya kuipatia Ugiriki fungu la pili la msaada wa kuiokoa nchi hiyo isifilisike ndiyo yaliyohanikiza magazetini hii leo.

https://p.dw.com/p/147Qd
Mwenyekiti wa zoni ya Euro Jean-Claude Juncker, Mkuu wa shirika la fedha la kimataifa Christine Lagarde na kamishna wa Umoja wa Ulaya anaeshughulikia masuala ya sarafu ya Euro Olli Rehn katika mkutano wa mjini BrusselsPicha: REUTERS

Tunaanzia na gazeti la Donaukurier linalojiuliza:Ndo kusema Ugiriki imeshanusurika? Hata kidogo.Mengi kati ya yaliyofikiwa jana usiku mjini Bruxelles yamefungamanishwa na masharti yasiyokadirika.Kubwa walilolipata wagiriki labda ni muda wa kuvuta pumzi.Hatari ya kufilisika imebakia pale pale.

Gazeti la "Sächsischer Zeitung" linajiuliza eti makubaliano hayo yanatosha kuwafanya wagiriki washukurie.Gazeti linaendelea kuandika:Licha ya makubaliano hayo,hakuna sababu za kutosha kuweza kushangiria.Hadi wakati huu fungu hili la pili la msaada,hatua za kupunguza madeni na zaidi kuliko yote mchango wa Athens katika kukabiliana na hali hiyo ni mambo yaliyomo karatasini tu.Hakuna bado anaeweza kuashiria kama wafadhili wote wa kibinafsi wataunga mkono yaliyofikiwa, kama vyama vya kisiasa nchini Ugiriki vitakuwa kweli na moyo wa kupitisha sheria husika na kama wagiriki watashukuria juhudi hizo kwa kuwachagua walio wengi bungeni.

Athen Krawalle
Machafuko mjini AthensPicha: AP

Maoni sawa na hayo yametolewa pia na gazeti la "Mitteldeutsche Zeitung" ambalo baada ya kujiuliza kama wapiga kura wa Ugiriki watawachagua wabunge wengi watakaounga mkono mageuzi,uchaguzi wa kabla ya wakati ukapaoitishwa April mwaka huu, linaendelea kujiuliza:Muhimu zaidi ni suala kwa jinsi gani watu wanaweza kuwa na uhakika kama fungu hili la pili la msaada litaleta tija zaidi kuliko la mwanzo?Nani anaedhamini kwamba jumla ya Euro bilioni 130 zitatumika ipasavyo na hazitapotea katika matundu yaliyo matupu.

Flagge EU Griechenland Fahne Symbolbild
Bendera ya Ugiriki na ile ya Umoja wa UlayaPicha: dapd

Gazeti la "Nordwest Zeitung linajishughulisha zaidi na uchaguzi utakaofanyika nchini Ugiriki na kuandika:Miezi ijayo kunafanyika uchaguzi nchini Ugiriki,Utafiti wa maoni ya umma unaashiria mabadiliko makubwa.Mageuzi hayo yanakihusu zaidi chama kikubwa cha kisiasa nchini humo- chama cha kisoshialisti.Kwa mujibu wa utafiti wa maoni ya umma,chama cha jadi-Pasok kinakabiliwa na hatari ya kuporomoka.Chama cha upinzani cha kihafidhina kinachohusika sawa na wasoshialisti katika janga la madeni linaloikaba Ugiriki,kinapigiwa upatu wa kuibuka na ushindi,ushindi unaoweza lakini kugeuka machungu.Hawataweza kutawala pamoja na kundi dogo la wasoshialisti.Bungeni pengine wataketi wafuasi wa siasa kali tu tangu za mrengo wa shoto mpaka zile za mrengo wa kulia.Wapinzani wakubwa wa uamuzi unaopitishwa na umoja wa Ulaya.Ugiriki inakabiliwa na kitisho cha kugeuka nchi isiyotawalika.Na kitakachofuata hapo ni nini?

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri:Josephat Charo