1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatimaye matumaini ya kuokolewa.

Abdu Said Mtullya9 Oktoba 2010

Wachimba migodi nchini Chile wafikiwa na mtaimbo maalum.

https://p.dw.com/p/PaEl
Ishara ya Maria mtakatifu inayotoa matumaini kwa wachimba migodi 33 walionaswa chini ya ardhi nchini Chile.Picha: AP

SAN JOSE:

Wachimba migodi 33 walionaswa chini ya mgodi sasa wamefikiwa na mtaimbo.

Mtaimbo huo ulichimba na kuingia katika sehemu waliponaswa wafanyakazi hao umbali wa futi alfu mbili chini ya ardhi. Na sasa itawezekana kutengeneza upenyo utakaowezesha kuteremsha kitasa maalumu kitakachowapakia watu hao na kuwafikisha juu ya ardhi. Mlio wa king'ora ulioashiria kufaulu kwa juhudi za kuwafikia wachimba migodi hao uliwapa faraja watu hao pamoja na ndugu zao nchini Chile kote.

Rais Sebastian Pinera wa Chile amesema, kile ambacho kingeliweza kuwa msiba sasa kimegeuka kuwa neema.Watu hao sasa wanatarajiwa kuuona tena mwanga wa jua katika muda wa siku chache zijazo.