1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAVANA: Fidel Castro aondosha wasiwasi kuhusu hali yake

22 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNi

Kiongozi wa Cuba,Fidel Castro mwenye miaka 81, ameonekana kwenye televisheni katika mahojiano ya kama saa moja,ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu takriban miezi minne iliyopita.Akizungumza pole pole,Castro ameondosha wasiwasi uliozuku kuhusu afya yake.Vile vile kulivuma kuwa ameshafariki dunia.Fidel Castro,alieshika madaraka katika mapinduzi ya mwaka 1959,hakuonekana hadharani tangu Julai mwaka 2006,alipofanyiwa upasuaji wa utumbo na kumkabidhi mdogo wake Raul Castro madaraka ya kuongoza serikali.