1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Heiligendamm: Kansela wa Ujerumani asifu mkutano wa G8

9 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtS

Kansela wa Ujerumani, Bibi Angela Merkel, ameusifu mkutano wa mataifa manane yaliyostawi kiviwanda, G8, akisema umefanikiwa na kwamba mataifa hayo makuu yameshughulikia ipasavyo masuala nyeti yaliyoyakabili.

Bibi Angela Merkel, ambaye pia anashikilia urais wa Umoja wa Ulaya, amesema wakuu wa mataifa hayo wameafikiana maswala mazito.

Viongozi hao waliojumuika katika mji wa kitalii wa Heiligendamm katika kikao cha siku tatu wamekubaliana kupunguza kwa kiasi kikubwa gesi zinazotoka viwandani.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, ameunga mkono matamshi ya Bibi Angela Merkel kwa kusema mikataba ya kimataifa itasaidia kuafikia lengo la kupunguza gesi hizo kwa asilimia hamsini ifikapo mwaka 2050.

Viongozi hao pia wameahidi kulipatia bara la Afrika msaada wa dola bilioni sitini za kukabiliana na homa ya malaria pamoja na Ukimwi na wakati huo huo kuzingatia ahadi waliyoweka hapo awali ya kuongeza fedha za kufadhili maendeleo barani humo.

Wanaharakati wa kutetea maendeleo wamelalamika kwamba mataifa hayo yametoa msaada kidogo sana kuzisaidia nchi maskini.