1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HEILIGENDAMM : Kauli za matumaini kwa mabadiliko ya hewa

6 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuM

Rais George W. Bush wa Marekani na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani wamekuwa wakitowa kauli za matumaini juu ya uwezekano wa kufikia makaubaliano juu ya mabadiliko ya hali ya hewa katika mkutano wa kila mwaka wa Viongozi wa Kundi la Mataifa Manane yenye Maendeleo makubwa ya viwanda duniani unaoanza leo hii katika mji wa Heiligendamm nchini Ujerumani.

Bush na Merkel walikutana katika chakula cha mchana leo hii kujaribu kupunguza baadhi ya tafauti zao kabla ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano huo wa siku tatu hapo jioni hata hivyo bado inaonekana kwamba hawaafikiani sana juu ya suala hilo.

Marekani imekiri kwamba kuongezeka kwa ujoto duniani ni tatizo kubwa sana wakati Ulaya imekuja kukubaliana na wazo la Marekani kwamba hakuna suluhisho linaloweza kupatikana bila ya watumiaji wakubwa wa nishati kama vile China,India na Brazil.

Pia wanakubali kwamba ukuaji wa uchumi hauwezi kutolewa muhanga kwa ajili ya kufikiwa maendeleo katika suala la mabadiliko ya hali ya hewa.