1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HEILIGENDAMM: Mji wa Heiligendamm wafungwa na polisi

30 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwg

Vikosi vya usalama hapa Ujerumani vimeufunga mji wa mapumziko wa Heligendamm katika bahari ya Baltic huku mkutano wa nchi za G8 ukikaribia kufanyika.

Ua mrefu wa sing´eng´e unaouzunguka mji huo yapata kilomita 12 unalenga kuwazuia waandamanaji wanaopinga utandawazi wasiwafikie viongozi mashuhuri duniani wataohudhuria mkutano huo wa mjini Heiligendamm.

Maafisa 16,000 wa usalama watatumwa kushika doria kukabiliana na waandamanaji takriban laki moja.

Usalama ni swala lililozusha mjadala mkubwa kwa sababu ya gharama yake ya euro milioni 12.5. Ijumaa wiki iliyopita mahakama ya Ujerumani ilibatilisha uamuzi wa kupiga marufuku maandamano katika eneo la kilomita tano la mji wa Heiligendamm.