1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Heiligendamm, Ujerumani. Heiligendam wafungwa.

31 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwS

Majeshi ya usalama ya Ujerumani yameufunga mji wa kitalii ulioko pwani katika eneo la Baltic wa Heiligendamm kabla ya mkutano wa wiki ijayo wa wakuu wa mataifa tajiri yenye viwanda duniani G8.

Ukuta mrefu wa waya za chuma wenye urefu wa kilometa 12 kuzunguka mji huo , unalengo la kuwazuwia waandamanaji wanaopinga utandawazi kufika karibu na viongozi ambao watahudhuria mkutano huo.

Maafisa wanasema kuwa kiasi cha maafisa wa usalama 16,000 watakuwapo ili kujitayarisha kwa mapambano na kiasi cha waandamanaji 100,000 wanaotarajiwa kuhudhuria katika mji huo.